Saturday, March 10, 2018

YAMENIFIKA

Mwezenu yamenifika, sikieni.
Hili jambo uhakika, bwabwajeni.
Nampenda kihakika, bi fulani.
Jina sikutajieni.

Chuoni hajapafika, msibuni.
Mkaanza paparka, ni Fulani.
Nampenda pasi shaka, ni mwandani.
Daima sitomuwacha.

Hilo munolitamka, ni uhuni.
Sio kila linozuka, midomoni.
Kuwa ndilo uhakika, fikirini.
Kabla ya kubwabwaja.

By Mfungwa huru

No comments:

Post a Comment