SEMA YANOUSHUHUDA
Naja kutia mkazo, kwa lile nilowambia.
Ila lisiwe tatizo, kukwaza wapita njia.
Yanoushuhuda mwanzo, yesema kiyapania.
Usiropokwe kijinga, ukome wako ulimi.
Sasa mmezidi mno, wezenu kufatilia.
Kazi yenu minong'ono, ya kwao kusimulia.
Ishara na kwa mifano, na mafumbo kutumia.
Usiropokwe kijinga, ukome wako ulimi.
Sijakwambia bwabwaja, kusema soshuhudia.
Au watu kuwataja, majina kuchafulia.
Ila uzitoe hoja, kwa ulioshuhudia.
Usibwabwaje kijinga, ikome yako midomo.
Sikuja kuwakomesha, natoa yenye udhia.
Ili mambo kuboresha, ya kwetu kufatilia.
Laleni au kukesha, msile msinywe pia.
*_Ila_*
Sema yanoushuhuda, siseme ya kusikia.
Naanza na Taimuri, umbea mekuzidia.
Zingatia ushauri, soyajua ulizia.
Usibwabwaje dhahiri, ya watu kuhadithia.
Sema yanoushuda, siseme ya kusikia.
Naungulia moyoni, Dillah wewe kukwambia,
Hashimu na da Mgeni, heshima nawapatia.
Ila haya yashikeni, yote niliowambia.
Sema yanoushuhuda, watu watakuelewa.
Na isiwe mada kesi, mpole sitomwambia.
Luti simwage kamasi, usoni kunirushia.
Kwake Bimu sina wasi, lakini namuwambia.
Siropokwe soyajua, yatakuja kukuponza.
Wahida yeye mbishi, haya atapuuzia.
Ataleta magumashi, na hata kuninunia.
Ila haliniyumbishi, ngangari nitabakia.
Sema yanoushuhuda, siseme usoyajua.
Khadija tunao wengi, kimya wamejikalia.
Hii sifa ya msingi, mola kawatunukia.
Kwao kubwabwaja kwingi, wameshajizuilia.
*_Ila_*
Pale mtapobwabwaja, sema yanoushuhuda.
Nachukua kihanjifu, majasho ninafutia.
Arafa sijekashifu, eti nakufatilia.
Sijaja humu kwa rafu, ugomvi kufuatia.
Mdomo wako uchunge, usije ukakuponza.
Mwisho kwa Mimi mtunzi, Ochu sijakamilia.
Wengi walinita tozi, jina kunichafulia.
Sifa yangu kurumbwizi, zuri shida kinijia.
Kibaya kwangu kichaka, pale nikijitokea.
Ila nikome kusema ovyo, Yale nisoshuhudia.
By Mfungwa huru
No comments:
Post a Comment