CHANGAMOTO NDO MAISHA
Naja tena kwa unyonge, kundini kuwakumbusha.
Mambo wazi nisifunge, ujumbe kuufikisha.
Yawaondoke mazonge, rohoni yanowarusha.
Hutoweza fanikiwa, bila kupata mazito.
Changamoto duniani, zipo pia zinafunza.
Zawafika insani, akili zao kukuza.
Watu sio punguwani, badala huzigeuza.
Ukijua changamoto, fanikio tatakuja.
Bila shaka hula mbivu, yule atovumilia.
Kuwacha wake uvivu, maarifa kutumia.
Pia kiwa muangavu, kwa mambo yalomjia.
Subira nguo adhima, ikiivaa hujuti.
Maneno sio mkuki, usiyajali ya watu.
Adui sio rafiki, akulae kama chatu.
Sisadiki wanafiki, kwao hutapat kitu.
Vazi la mtu tabia, utu si sura sikia.
Changamoto ninasema, shida tabu matatizo.
Iweke subira njema, itoe yako mizozo.
Ngangari simama wima, maisha ndo lako funzo.
Njia za mafanikio, changamoto na subira.
Sita beti zimetimu, inatosha kuhubiri.
Subira kitu muhimu, usijifanye jabari.
Usije kunilaumu, tayari 'shakupa siri.
*_TENA_*
Sio kila ufanyalo, wengi litawavutia.
By mfungwa huru
No comments:
Post a Comment