Saturday, March 3, 2018

WARINGAO


Muringao matajiri, mukafurahia mali.
Akujieni fakiri, mwamsukumia mbali.
Hili jambo sio zuri, zikumbukeni asili.
Hakuna mkamilifu, waringao nawambia.


Waringao kwa viriri, kutoa sauti kali.
Mengi wanayahubiri, kutekeleza muhali.
Kwao waona fahari, ila kwetu idhilali.
Yaepukeni machafu, unafiki punguzeni.


Waringao kwa uzuri, umbo na sura jamali.
Wakavifanya viburi, wengine kuwadhalili.
Wajue kuna hatari, wasisahau ajali.
Hakuna mkamilifu, waringao nawambia.


Muringao nyie wari, akija mume kikweli.
Mnayapinga mahari, sababu za kijahili.
Muko radhi takriri, zinaa iwe amali.
Yaepukeni machafu, waringao nawambia.


Waringao kwa umri, pumzi za mola jalali.
Leo nawatahadhari, yatie kwenye akili.
Kuna siku itajiri, kutengwa roho na mwili.
Hakuna ataebaki, waringao nawambia.

Litaendelea


By Othame

Mfungwa huru

No comments:

Post a Comment