🌷SUBIRI🌷
Habari tumezipata, kuwa yeye aolewa.
Shairi hili matata, wengi litawasumbuwa.
Muwaliko kafumbata, wala hatukuwambiwa.
Pole usihuzunike, simanzi ukajitia.
Hawakukosea watu, maneno kuyatamka.
Kisichoridhiki katu, kwako hakyezi kulika.
Hebu tunza wako utu, ewe mwana msifika.
Maisha safari ndefu, yako ridhiki tapata.
Nilizani zako shere, maneno ulonambia.
Nikayapuuzia bure, sikioni kuyatia.
Mithili kipurepure, upeponi kujongea.
Pole usihuzunike, kumbe kweli aolewa?.
Zimeandikwa mbinguni, ndoa zote na manani.
Usifanye kisirani, ni mtu si hayawani.
Hebu kuwa subirani, utampata mwandani.
Subira subiri chako, mola alokuwekea.
Ituwe akili yako, ipoe na itulie.
Usijefanya vituko, ukaona ujiue.
Yupo wa ridhiki yako, fumba jicho usilie.
Sijui hisia zako, nakuomba vumilia.
Japo alikudanganya, simuwekee kinyongo.
Maneno akakuponya, nawe ukatoa hongo.
Yasahau nakukanya, utakwenda songombingo.
Urafiki ubakie, chuki usimuwekee.
Kutendwa kunaumiza, hilo mimi nalijua.
Mwana nimeshakufunza, ni vyema kusubiria.
Usijeukayabeza, yote niliyokwambia.
Subiri yako ridhiki, mola aloiyandika.
Nimefika kituoni, nanyamaza nisinene.
Jeraha lako moyoni, litibike na lipone.
Usipunguwe mwilini, uzidi wako unene.
Subirini wangu wana, ndoa zimeshaandikwa.
_*by mfungwa huru*_
No comments:
Post a Comment