BILA WEWE
Yaani wewe!, Uliyefanya jina langu likatukuka.
Si mwenginewe, uniokotae pale ninapoanguka.
Na *_bila wewe_*, duniani daima nisingetambulika.
Ndie wewe!, uliyenifanya Tungo nikaiandika.
Si mwenginewe, ila wewe ubongo wangu umeuteka.
Na *_bila wewe_*, furaha yangu duniani ingetoweka.
Haswa! Wewe, uyakosapo mafuta maji hunipaka.
Huna kiwewe nikikukosa hujawahi kasirika.
Na _*bila wewe*_, tabu nyingi nayo mashaka yangenifika.
Ibaki wewe, ninapotukanwa moyo wako huungulika.
Sifa upewe, hujawahi nibagua katika kila rika.
Na *_bila wewe_*, nisingelijua lipi jema la kushika.
_*by Ochu*_
_*Mfungwa huru*_
No comments:
Post a Comment