Saturday, March 10, 2018

NJIWA ASOHURUMA

Njiwa kwangu katuwa, kilipo chagu kidonda.
Kidonda chataka sawa, afurahi nikikonda.
Kanipiga lake bawa, pale kilipo kidonda.
Njiwa asonahuruma, kwa kweli kanitonesha.


Siku ya pili akaja, na hasira nyingi sana.
Kanipiga dono moja, dono lino kubwa sana.
Damu ikaanza vuja, kweli anitesa sana.
Njiwa asonahuruma, kwa kweli anitonesha.


Dawa yangu ipo kwake, anajuwa kwa undani.
Kikweli mateso yake, ni kama ya hayawani.
Ila kusudio lake, kunitia mtihani.
Njiwa asonahuruma, kwa kweli anitonesha.


Siku nyingi zikapita, na miezi kujongea.
Dawa nikaitafuta, ila sijaivumbua.
Nikabaki nnatuta, pumzi za mwisho kutoa.
Njiwa asonahuruma, kwa kweli anitonesha.


Nikapoteza uhai, kwa yote yake mashaka.
Njiwa kweli ni adui, kaburini kaniweka.
Nikazikwa niko hai, tena njiwa karidhika.
Njiwa asonahuruma, kwa kweli kafanikiwa.


_*by ochu*_

_*mfungwa huru*_

No comments:

Post a Comment