MAMBO NA WATU
Naja kwenu wanatungo, malenga mulo wachanga, hili neno si uongo, ndio mana nikatunga.
Tusafishe zetu nongo, tusije tukaboronga.
Mambo na watu jamani, mtu lake hataleza.
Mambo na watu jamani, mtu lake hataleza.
Hata ni rahisi kwani, au gumu likikwaza.
Tuwe pamoja gizani, hata mwanga kichomoza.
Mambo na watu sikia, mtu lake hataleza.
Mambo na watu sikia, mtu lake hataleza.
Kujitenga nakwambia, wengine watakukweza.
Shirikio ukitoa, nawe watakuliwaza.
Mambo na watu jamani, mtu lake hataleza.
_*Mfungwa huru*_
No comments:
Post a Comment