Saturday, March 10, 2018

DONGE

Siambi mimi hodari, wanatungo mwatambua.
Wala sitafuti shari, shairi kulitungia.
Ila neka hafikiri, wazo lililonijia.
Ipi maana sahili, ya neno *_donge_* jamia.

Yahangaika suduri, majibu kutafutia.
Maana ilo shuwari, ya neno donge jamia.
Nami bila ya hiari, leo ninaulizia.
Ipi maana halisi, ya neno *_donge_* jamia.

Donge naweka rohoni, nyongo inaponibana.
Donge machungu moyoni, utaponikera sana.
Donge ni fundo kooni, kinikera nakuchana.

Donge ni zonge la uzi, lililozongwa vizuri.
Kwa kireli kilowazi, na madhubuti hatari.
Kizongoa huwa kazi, usipokuwa mahari.

Donge pia ni finyango, yabisi ni yake hali.
Donge finyango la dongo, lilosokotwa sahali.
Donge dawa si uongo, kwa maradhi mbalimbali.

Donge la chumvi jamani, hili nalo tutambue.
Donge halina thamani, shimmia uuziwe.
Donge hutiwa chunguni, chakulani likolee.

Donge ndani mna nini?, mana limesokotana.
Donge lina siri gani, mbona mnalitukana.
Donge liko taabani, mapande limeachana.

Donge ni kijiji chema, kwao baba nae mama.
Donge mejaa neema, kairuzuku karima.
Donge nasema salama, ugomvi sio heshima.

Donge ninaweka tama, mbele sitoendelea.
Donge nimeshasimama, majibu kusubiria.
Nyote na mufanye hima, sudurini weze poa.
Ipi maana halisi, neno *_donge_* jamia.

_*by mfungwa huru*_

No comments:

Post a Comment