_*KIZAZI*_
Kizazi hiki kizazi, kizazi kimashakani.
Kizazi hiki chagizi, kizazi ka hayawani.
Kizazi?
Kizazi hiki kizazi, kizazi kifirauni.
Kizazi hiki kibwenzi, kizazi kiuzunguni.
Kizazi?
Kizazi hiki kizazi, kizazi chetu nyumbani.
Kizazi ni kidokozi, kizazi kihamkani.
Kizazi?
Kizazi hiki kizazi, kizazi kipo shidani.
Kizazi kifaraguzi, kizazi mitandaoni.
Kizazi?
Kizazi hiki kizazi, kizazi kilimbukeni.
Kizazi ki kama mbuzi, kizazi kiokoweni.
Kizazi?
Kizazi kile kizazi, kizazi kilo zamani.
Kizazi kile azizi, kizazi kirudisheni.
Kizazi!?
_*Mtunzi : Othman Ame Hamza.*_
_*Mshairi wa Donge*_
No comments:
Post a Comment