🌷WASIFAZO SIMPATI🌷
Hali yangu niko fiti, mzima wa afya pia.
Naiomba hidayati, mola niongoze njia.
Pia nyingi hasanati, za akhera na dunia.
Wasifazo simpati, nitamaliza dunia.
Uzuri wako banati, weupe wa asilia.
Na wekundu samawati, maji kunde mithilia.
Tabia zako thabiti, vyote vimenivutia.
Wasifazo simpati, nitamaliza dunia.
Punguza uafiriti, yangu kauli sikia.
Nikuonapo sijuti, moyo wangu hutulia.
Kwako raha mi sipati, machoni sipokutia.
Wasifazo simpati, nitamaliza dunia.
Mambo yapo jaharati, tena unayatambua.
Kuwa kwako nimeketi, moyo nimekuachia.
Uendapo udhibiti, ruhusa mekupatia.
Wasifazo simpati, nitamaliza dunia.
Upendo wangu wa dhati, kidondani meozea.
Kwako niko mahatuti, wewe wa kuniokoa.
Kama kwako si bahati, ujue nitajiua.
Wasifazo simpati, nitamaliza dunia.
Nimefikia tamati, shairi namalizia.
Pendo lako ni bahati, kamwe sitalichezea.
Nitaomba ghufirati, pale nikikukosea.
Wasifazo simpati, nitamaliza dunia.
🌷by ochu🌷
MFUNGWA HURU
No comments:
Post a Comment