SHAIRI
NANYAMAA
Kimya nanyamaa, midomo nabana.
Sitachachamaa, yenu kuyanena.
Midomo lemaa, tena koma sana.
Leo nanyamaa,
Sitaki umbea.
Ulimi vuata, nakuwasa sana.
Bora kuufyata, sijepata lana.
Pia kukupita, yasionamana,
Leo nanyamaa,
Sitaki umbea.
Meno bora uma, nisiwe naguna.
Koo madhuluma, kauka kuchuna.
Tamati kuguma, tiba si ruzuna.
Leo nanyamaa, sitaki umbea.
Siwi mzandiki, kuboboka sina.
Hawasharifiki, kukupa majina.
Hata marafiki, huzusha fitina.
Leo nanyamaa, sitaki umbea.
Naogopa chuki, tukaekeana .
Majungu lukuki, kuja kusutana.
Nazo taharuki, zikalimbikana.
Leo nanyamaa, sitaki umbea.
_*Mfungwa huru*_
Kwa maoni zaidi 👇
Usisahau kulike na kutoa maoni yako hapo chini
Au kupitia
othame10@gmail.com
0776820608